Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

MATIC AFUZU VIPIMO VYA AFYA

Picha
Kiungo Nemanja Matic amefuzu vipimo na muda mchache atatangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Man United. Matic anatoka Chelsea kujiunga na Man United kwa mkataba wa thamani ya pauni million 31. Raia huyo wa Serbia amekuwa chaguo namba moja la Kocha Jose Mourinho tokea akiwa Chelsea na sasa ametua Man United amefanya juu chini kuhakikisha anamnas

TABIA 5 ZA MSINGI ZITABORESHA MAISHA YAKO

Picha
Tabia ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Ukijenga tabia njema uwe na uhakika utafanikiwa na kufika mbali sana kimafanikio. Leo nataka tuangalie kupitia makala haya, tabia ambazo ukizifuata na kuzitekeleza zitafanya maisha yako kuwa bora na ya thamani kila iitwapo leo. 1. Usifanye kazi mbili kwa wakati mmoja . Mawazo yako yote weka kwenye kitu kimoja unachokifanya. Ukiweka mawazo kwenye vitu viwili, utashindwa kuvifanikisha vyote kwa ufasaha na utashindwa. 2. Usigombane na mtu mpumbavu . Kama kimetokea kitu cha kutoelewana na mtu ambaye unamwona hajielewi, achana naye ili asije akakupotezea muda wako bure. 3. Usiingie kwenye mabishano yasiyo ya lazima . Fanya kile unachokiamini, kubishana kwingi na kujaribu kuonyeshana eti nani ni mshindi ni mambo ambayo yanapoteza muda wako pia. Epuka kubishana. 4. Usifanye maamuzi bila ya kufikiri sana . Kama unataka kufanya maamuzi bora na ya maana kwako, yafanye kile kipindi ambacho akili yako imetulia, ukifanya maamuzi kwa harak...

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA NDOA

Picha
1. kucheka pamoja Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote. 2. Jifunzeni kutiana moyo Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele ya wengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi w...

MAMBO 13 USIYOYAJUA KUHUSU NYANGUMI

Picha
1. Moyo wa nyangumi una kilo 600. 2. Mtoto wa nyangumi ananyonya lita 600 kila siku ikiwa ni mwaka wa kwanza tu. 3. Mtoto wa nyangumi anakuwaga na uzito wa ki 2700 ambao ni sawa na kifaru mkubwa saizi ya mwisho. 4. Uzito wa nyangumi mkubwa unakadiriwa kuwa na tani 200 adi 300 mmoja jike alikamatwa na kupimwa alikutwa na kilo 171000. 5. Ulimi wa nyangumi una uzito wa tani 3 ambao ni uzito wa tembo mkubwa. 6. Mdomo wa nyangumi unauwezo wa kuifazi tani 90 za chakula na maji akiufungua mpaka mwisho. 7. Chakula kikubwa cha nyangumi ni dagaa kamba, ambapo nyangumi mkubwa hula dagaa kamba zaidi ya 4000000 kwa siku. 8. Ili nyangumi ashibe zaidi anakula kilo 3600. 9. Nyangumi anaweza kuishi miaka zaid ya 250. 10. Baazi ya mishipa ya nyangumi ni mikubwa kiasi kwamba binadamu anaweza kuogelea ndani ya mishipa hiyo bila kugusa gusa pembeni. 11. Ukubwa wa nyangumi unaweza kuwa zaidi ya ndege aina ya ‪#‎boeing‬ 12. Urefu wa nyangu unakadiriwa kuwa mita 30mpaka 50 uki mu...

MADHARA 6 YA KUTOA MIMBA

Picha
Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake. Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba. Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu? Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe...

PSG YAPANIA KUVUNJA REKODI YA USAJILI KWA NEYMA

Picha
Katika kuonesha jeuri ya pesa matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu ya PSG wamepiga hodi katika klabu ya Barcelona tayari kwa ajili ya kuvunja rekodi ya dunia kumtwaa mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar. Taarifa zinasema kiasi cha zaidi ya £200m ambayo ni mara mbili na zaidi ya pesa zilizotumika kumnunua Paul Pogba ambaye kwa sasa ndio anashikilia rekodi ya usajili ya dunia kwa sasa. Ripoti zinasema klabu ya PSG inataka kutumia mwanya wa Neymar kukosa uhuru wa kucheza free mbele ya Messi hivyo wanataka kutuma ofa ya karibia £222m ambayo ni wazi itawashawishi Barcelona kumuuza. Katika dili hiyo Neymar atakula £30m kila mwaka na uwepo wa Dani Alves katika kikosi cha PSG unaweza kuwa ushawishi mkubwa kwa Neymar na PSG wanaweza kumtumia mlinzi huyo kumshawishi Neymar. Habari zinasema Neymar hana furaha na Barcelona kwani ni ngumu kuchukua tuzo ya Ballon D’Or ukicheza mbele ya Suarez na Messi ambapo washambuliaji hao wanaminya uhuru wa Neymar akiwa uwanjani. Lakini k...

TAMBUA JINSI YA KUKABILIANA NA MINYOO INAYOLETA MAGONJWA

Minyoo ni viumbe hai ambavyo husababisha madhara ya kiafya kwa mtu aliyeambukizwa. minyoo huishi na kukua katika utumbo ambamo hufyonza virutubisho ambavyo ni muhimu kwa lishe ya binadamu.aina ya minyoo inayosababisha kichocho huishi katika kibofu cha mkojo. Minyoo kwenye utumbo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kudhoofisha lishe ya binadamu,hupunguza uwezo wa mtu wa kufanya kazi,udumavu wa akili na madhara mengine. Minyoo ya tumbo inayomwathiri mwanadamu ni pamoja na minyoo mviringo.minyoo ya safura,minyoo mjeledi,ninyoo sindano,minyoo uzi na tegu. Dalili za uambukizo wa minyoo ya kwenye utumbo ni : 1. Kuwashwa mwili na sehemu ya haja kubwa. 2. kukohoa kikohozi kikavu 3. kukosa hamu ya kula 4. kuumwa tumbo na wakati mwingine kuharisha. 5. Udhaifu wa mwili na kuckoka kwa mara kwa mara 6. Kuvimba tumbo. 7. Kutapika 8. Utumbo kutoka nje ya unyeo 9. Kutoa minyoo kwa njia ya haja kubwa, kutapika minyoo au minyoo kutoka puani. 10. Kizunguzungu 11. Kupauka kwa fizi, uli...

LOWASA ATANGAZA USHINDI 2020

Picha
Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema licha ya changamoto nyingi anazopata akiwa ndani ya upinzani, atagombea tena urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na anaamini atashinda. Lowassa aliyejitokeza kugombea urais kupitia CCM mwaka 2015 na jina lake kukatwa kisha kuhamia Chadema alikogombea nafasi hiyo akiwakilisha vyama vilivyoungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kushindwa na Rais John Magufuli. Bado anatajwa kuwa mgombea mwenye nguvu katika kambi ya upinzani. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rais Magufuli alishinda kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46, huku Lowassa wa Chadema akijipatia kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote. Akizungumza jana katika mahojiano maalumu na waandishi wa Nation Media Group (NMG) jijini Nairobi, Lowassa alisema, “Kwa mapenzi ya Mungu nitajaribu tena mwaka 2020 na nitapita kwa mikono safi.” Kama ambavyo amekuwa akisema tangu aliposhindwa katika u...

MWIGULU ATANGAZA AJIRA NYINGI

Picha
Akizungumza jana wakati wa kikao cha kujadili utendaji ndani ya jeshi hilo, Mwigulu alisema katika mwaka wa fedha wa 2017/18, serikali imepanga kuajiri askari wapya 600 ndani ya jeshi hilo ikiwa mkakati wa kupunguza uhaba wa watumishi ndani ya chombo hicho. Kutangazwa kwa ajira hizo, ni mwendeleo wa serikali katika kuhakikisha inapunguza tatizo la watumishi serikalini ambako kwa sasa kuna uhaba mkubwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuondolewa kwa wale waliobainika kuwa na vyeti feki. Juzi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alitangaza ajira mpya 10,000 kwa watumishi wa kada mbalimbali kwa ajili ya kufidia pengo hilo. Waziri Mwigulu alisema, ndani ya Zimamoto na Uokoaji, serikali imedhamiria kushughulikia masuala ya kisheria, maslahi na yale ya kiutendaji ili kulifanya kuwa na hadhi sawa na majeshi mengine yaliyoko chini ya wizara hiyo. Akifungua kikao hicho cha siku mbili, alisema serikali inatambua changamoto zin...

NJIA 5 ZINAZOMUONYESHA MUME AU MKE ASIYEFAA

Picha
Kuna watu wenye tabia mbaya kiasi kwamba wapenzi wao wanajuta kuoana nao, wanaona ni heri zaidi kama wangeishi peke yao. Sasa, utamjuaje mwanaume au  mwanamke mwenye tabia mbaya, ili ujiokoe na ndoa yenye utata? 1. Tabia zake haziendani na wewe . Kama tabia zako haziendani na mwanaume au mwanamke unayetaka kuoana naye, ujue mapema ya kuwa ndoa yenu itajaa mfurulizo wa matatizo bila kukoma na hivyo mtadumu katika migogoro na ugomvi usioisha. 2. Huishusha hadhi yako mbele ya familia na rafiki zake . Atakuwa mume au mke mbaya kama umegundua tabia yake ya kupenda kuishusha hadhi yako mbele ya familia au rafiki zake. Hasa kama ni mwepesi wa mapungufu yako mbele ya rafiki zake, hata kabla hajakwambia lolote juu ya udhaifu wako, unamkuta mtu mzima anadiriki hata kuwaeleza rafiki zake juu ya udhaifu wako faragha, ukimjua huyo usithubutu ndoa.Ana sifa hizi 5? Usikubali ndoa 3. Hawakubali wana familia na rafiki zako . Kama anakuwa mtu wa kusimamisha bendera nyekundu (r...

ROONEY AFUNGA GOLI LA KWANZA TANGU AJIUNGE NA EVERTON LEO

Picha
Mpira umekwisha kwa Everton kushinda bao 2-1, magoli yakifungwa na Rooney dakika ya 35 kabla Tuyisenge wa Gor Mahia kusawazisha dakika mbili baadaye. Goli la ushindi la Everton limepatikana dakika ya 82 kupitia kwa Dowell. Hata ivyo mashabiki walifurika kiwanjani hapo kumshuhudia Wayne Rooney

PUTIN NA TRUMP MAMBO SAFI

Picha
Putin na Trump walikutana mjini Hamburg Rais wa Marekani Donald Trump anasema anaelewana vyema na rais wa Urusi Vladimir Putin. Alihojiwa na kituo cha Christian Broadcasting Network, siku chache baada ya mkutano uliokuwa ukisubiriwa kati yake na Putin wakati wa mkutano wa G20 mjini Hamburg. Trump pia amesema kuwa alikuwa na uhakika kuwa Putin angependa Hillary Clinton akiwe madarakani Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa. Trump anakana kufahamu hilo na Urusi nayo mara kwa mara imekana kuingilia kati. "Sisi ni nguvu kubwa ya kinuklia, sawa na Urusi. haitoi maana yoyote ikiwa tutakosa kuwa na uhusiano." Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa. Bwana Trump alitaja usitishwaji wa hivi majuzi wa mapigano kusini magharibi mwa Syria kama njia moja ya kuonyesha ushirikiano na Bwana Putin. Trump pia alitumia mahojiano hayo kukana madai kuwa Urusi ilichangia kuchaguliwa kwake. Mapema Trump alimtetee mwan...

NAFASI ZA AJIRA LEO 13

Picha
Bonyeza Links Zifuatazo kusoma zaidi na kuapply: Job Opportunity at Wakulima Tea Company Ltd, IT System Administrator (IT) 5 Job Opportunities at Feza International Schools Job Opportunity at High Commission of CANADA In Tanzania, Common Service Assistant Job Opportunity at DUMA Works, Office Administrator Job Opportunity At IntraHealth, Supply Chain Senior Officer 53 Job Opportunity at SUNSHARE Investment Ltd, Sales Representatives 10 Job Opportunities at Air Tanzania Company Limited (ATCL) Kwa maelezo zaidi ingia: www.ajirayako.com

DALILI ZA KUMJUA RAFIKI AMBAYE NI MSALITI

Picha
Rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi yakiwemo 1.Kwenye mapenzi 2.Kwenye biashara 3.Kwenye kupata nafasi kazini  4.Kwenye mahusiano na marafiki zenu 5.Kwenye mikataba au tenda Dalili / Mazingira -Unasikia au unagundua anakusema vibaya kwa wengine, tofauti na akiwa na wewe. - Unahisi au unagundua anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani. - Unahisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako. -Unahisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni Unafanyaje?. -Usimwamini sana mtu wa namna hii. - Usijiachilie na kuwa wazi sana kwa mtu huyu. -Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia.

KWANINI WANAWAKE WENGI HAWAOLEWI KWA WAKATI

Picha
Kuoa au kuoelwa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha. Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kutokuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana. Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa. 1. Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii . Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine. Kutwa nzima unakuta ana...

NGELEJA AZUA MIJADALA

Picha
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitangaza hivi karibuni kurudisha Tsh. mil 40.4 alizopewa na mfanyabiashara James Rugemarila ambaye anahusishwa na tuhuma za ESCROW na kuibua mijadala katika jamii. Hatua ya Ngeleja kurudisha fedha hizo imeibua mijadala mbalimbali katika jamii ambapo watu mbalimbali waikiwemo Wanasheria wamekuwa wakiizungumzia issue hiyo ambayo tayari baadhi ya wahusika wamefikishwa Mahakamani akiwemo Rugemarila na kusomewa mashtaka. Miongoni mwa wanasheria hao ni Hashimu Mziray ambaye anasema alichokifanya Ngeleja ni udhaifu na anatakiwa kuomba radhi, kwani fedha hizo alizichukua muda mrefu na huenda alizifanyia uzalishaji ambapo kisheria halijakaa sawa.

GAZA HAPAKALIKI

Picha
Umoja wa Mataifa umesema Ukanda wa Gaza haukaliki kwa wakazi wake wapatao milioni mbili. Katika ripoti inayoangalia hali ya kibinadamu, -Umoja wa Mataifa umesema kiwango cha kipato. -huduma ya afya. -Elimu. -Huduma ya umeme na maji safi ya kunywa imezorota katika kipindi cha miaka kumi tangu Hamas ichukue madaraka katika eneo hilo. Baada ya kuchukua utawala, Israel ambayo inaitambua Hamas kama kundi la kigaidi, ikishirikiana na Misri wameitenga Gaza. Mamlaka ya Palestina, ambayo inadhibiti eneo la West Bank imesitisha uhamishaji wa fedha katika ukanda huo wa pwani na kuitaka Israel kupunguza huduma ya umeme.

JUA MADHARA YA SARATANI YA DAMU

Picha
Leukemia ni Saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima. Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali. Leukemia husababishwa na nini Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira. Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake...

UFUGAJI WA NGURUWE

Picha
Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000 - Banda la mabanzi=1,000,000 - Chakula = 1,000,000 - Dawa= 200000 After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100, mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000. After 2yrs : Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike). Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500. 1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil. Welcome to the club Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu. 1. Kwanza tambua hii ni agri-business,basi kama business nyingine inahitaji usimamizi wa kutosha. Watu hudhani ukianzisha mradi na kuweka kijana wa kuwalisha basi unangojea faida tu. Ni vema ukaelewa mahitaji ya hao wanyama (chakula,usafi,m...

LUKAKU ASAJILIWA RASMI MAN UNITED

Picha
KLABU ya Manchester United imefanya usajili wa pili dirisha hili, baada ya kumnasa mshambuliaji hatari, Romelu Lukaku anayevunja rekodi ya dau kubwa la usajili. Kukamilika kwa dili hilo inamaanisha kocha Mreno, Jose Mourinho ameipiku klabu yake ya zamani, Chelsea katika vita ya kuwania saini ya Mbelgiji huyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anahamia Old Trafford kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 75 - inayomfanya awe mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka ya Uingereza. Lukaku amesaini mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja zaidi. "Ningependa kuanza kuwashukuru Everton na mashabiki kwa misimu minne ya aina yake iliyopita, nimetengeneza marafiki fulani maalum na tumekuwa na wakati fulani mzuri pamoja," amesema Lukaku na kununukuliwa na tovuti ya United. "Pamoja na hayo, wakati Manchester United na Jose Mourinho wanakuja kugonga mlango ni fursa nzuri maishani ambayo nisingeweza kukataa," amesema. "Unaweza kuona mpamban...

LULU ARUDI SHULENI

Picha
MAMA mzazi wa staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila amezima minon’gono ya mwanaye huyo kutarajia kufunga ndoa akisema kuwa, mtoto wake huyo anajipanga kurudi darasani kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo. Akizungumza na Wikienda, mama Lulu alisema kuwa, kama mwanaye huyo angekuwa anaolewa kila mtu angejua kwa sababu ni jambo jema. Lakini kwa sasa Lulu anajipanga kurudi Chuo cha Magogoni kilichopo Posta jijini Dar, kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya diplomasia. Hii ina maana kuwa elimu haina mwisho na kushauri wasanii mbalimbali wajiendeleze na masomo.

MUGABE ATEULIWA TENA KUGOMBEA URAISI

Picha
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejelea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu. Hata ivyo kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kuenda Singapore kwa matibabu. Gazeti la kibinfasi la News Zimbabwe lilimnukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC akisema. "yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu sio nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili. Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya." Karauone Chihwayi, msemaji wa upande uliojitoa MDC naye alitoa matamshi kama hayo. "Nchi hii imekwama leo hii kwa sababu rais wa Zanu anaongoza akiwa kitanda cha hospitali." Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.

UGONJWA WA KISONONO HATARI KWA MAISHA

Picha
Shirika la afya Duniani, WHO, limetoa tahadhari kuwa, ugonjwa wa zinaa wa kisonono, umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa ya kupambana na ugonjwa huo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mataifa 77 tofauti Duniani. WHO imebaini kuwa maambukizi wa ugonjwa huo nchini Japan, Ufaransa na Uhispania, hayatibiki kabisa. Lakini hata hivyo, shirika hilo linasema wengi wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi masikini, ambazo zinavifaa duni kudhibiti ugonjwa huo. Shirika hilo la Afya duniani linasema kufanya mapenzi bila ya kuingiliana na watu wachache wanaotumia kondomu kunasaidia kuenea kwa ugonjwa huo wa Kisonono.

MOTO WATEKETEZA SOKO NCHI ZAMBIA

Picha
Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangaza hali ya dharura nchini humo kutokana na moto mkubwa uliyotekteza soko kuu la mjini Lusaka. Moto huo pamoja na visa vingine kama hivyo unadhaniwa kuanzishwa kwa maksudi na rais Lungu anasema ni vitendo vya kuhujumu uchumi ili kuifanya Zambia isitawalike vyema. Hata hivyo wapinzani wake wanasema Rais Lungu anatumia mikasa hiyo kama kisingizio cha kuendeleza utawala wa kiimla.

ARSENAL YASAJILI MSHAMBULIAJI

Picha
Timu ya Arsenal imekamilasha usajili wa mchaeza lacazzete kutoka Lyon nchini ufaransa. Alexander laccazzete amekuwa mchezaji ghali katika kipindi hiki.

JUA VYAKULA VINAVYOOGEZA UWEZO WA AKILI

Picha
Katika mwili wa mwanadamu hakuna kitu chenye umuhimu mkubwa kama ubongo, ubongo ndio ambao humsaidia mwanadamu katika kufanya mambo mbalimbali, hata hivyo inaelezwa ya kwamba ubongo wa mwanadamu ndio humfanya mwanadamu kuonekana hivyo alivyo. Hivyo inaelezwa ya kwamba ili mwanadamu aweze kuongeza akili, katika kufikiri na kutenda mambo mbalimbali anatakiwa kula vyakula vifuatavyo: Mafuta ya samaki . Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama sangara na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja. Ulaji wa mbegu za maboga . Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, huweza kusaidia ku...

JINSI YA KUWA TAJIRI

Picha
BILA shaka ukiulizwa leo kama unataka kuwa tajiri, jibu lako litakuwa ni NDIYO! Lakini je, tunaelewa maana ya utajiri na namna ya kuwa tajiri? Hili ni swali ambalo majibu yake yanawasumbua wengi. Mada hii itakusaidia kupata mwanga wa maana na namna ya kuutafuta utajiri. Wengi wanaamini kuwa ili mtu awe tajiri lazima awe na bahati ya kipekee. Watu wengi hudhani kuwa hawawezi kuwa matajiri mpaka watumie mizizi ya Bagamoyo, Tanga au Sumbawanga. Wengine huamini kwamba ili uwe tajiri, ni lazima uoe au uolewe na tajiri. Zipo imani nyingi juu ya utajiri, wengine wanaamini lazima uwe na ‘zali', ufanye biashara ya magendo, ukwepe kodi, uibe, utoe uhai wa mtu au utumie njia nyingine haramu ndiyo uupate utajiri. SIRI YA UTAJIRI HII HAPA Siri kubwa ya mtu kuufikia utajiri wa kweli na wa kudumu, ni kuanzisha biashara yenye faida ambayo utakuwa na uwezo wa kuimiliki na siyo biashara ikumiliki wewe. Ukifanikiwa kuanzisha biashara yako, jambo la muhimu kuliko yote ni kuhakikisha una...

MAONYESHO YA SABASABA YAONGEZEWA MUDA

Picha
Maonyesho ya Sabasaba mwaka huu yanoga Rais John Magufuli amepeleka neema kwa wananchi wanaoshiriki maonyesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba baada ya kupendekeza kuongezwa kwa siku tano zaidi. Maonyesho hayo yaliyoanza rasmi Juni 28 na kutarajiwa kumalizika Julai 8, sasa yatamalizika Julai 13, mwaka huu na kutimiza siku 16. Akifungua maonyesho hayo jana, Jumamosi, jijini hapa, Rais Magufuli alimwomba Mwenyekiti wa Bodi ya Biashara (Tantrade) afikirie kuongeza siku ili wananchi waweze kushiriki kwa muda mrefu zaidi. “Kama likiwagusa, waongezeeni muda wananchi washiriki kwa muda mrefu zaidi, muwape nafasi taasisi za kujifunza zaidi,” alisema na kuongeza: “Ni siku muhimu sana katika maendeleo ya Tanzania, haya ni maonyesho yangu ya kwanza kama mualikwa, mwaka jana mgeni rasmi alikuwa mwingine mimi nilikuwa msindikizaji.” Kutokana na pendekezo hilo la Rais, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantr...

TAJIRI ATUMA SHEHENA YA BENDERA 5000 ZA CHILE KWA AJILI YA FAINALI LEO

Picha
Tajiri awapa mashabiki wa Chile bendera 5,000 kwaajili ya fainali leo Mwanabiashara mmoja tajiri nchini Chile ametuma shehena ya bendera elfu tano huko Urusi ambako timu ya taifa lake Chile inapambana na Ujerumani katika mechi ya fainali ya kombe la mashirikisho inayochezwa baadae leo huko St Petersburgs . Ujerumani ndio mabingwa wa sasa wa kombe la dunia. Mfanyibiashara huyo wa madini, Leonardo Farkas katika ujumbe wake alioutuma kupitia akaunti yake ya facebook, amewahimiza mashabiki wa Chile nchini Urusi kukusanyika nje ya hotel waliko timu ya Chile, wakati wa saa za chakula cha mchana, ili kuwatakia ushindi na vilevile kupokea viji-bendera hivyo vidogo ambavyo wanavipeperusha wakishabikia na kushangilia. Mbali na mechi hizi za kombe la shirikisho Urusi itakua pia wenyeji wa kombe la dunia mwaka ujao kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Hii si mara ya kwanza mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 50 ametoa pesa nyingi kuipa motisha timu hiyo ya Chile. Mwak...

NORWAY YAIPATIA TANZANIA DOLA 1O.5 ZA KIMAREKANI

Picha
Norway yaipatia Tanzania Dola Milioni 10 Nukta 5 za Kimarekani Bunge la Tanzania limesoma miswada mitatu inayohusu rasilimali za maliasili za nchi Sirro: Ushirikiano wa dhati baina ya wananchi na dola unahitajika kukomesha mauaji Pwani. Taifa Stars kumenyana na Afrika Kusini katika robo fainali ya COSAFA Ujerumani na Chile zatinga fainali ya michuano ya kombe la mabara Posted : July 02, 2017 (today) By Costamalimbwi Norway yaipatia Tanzania Dola Milioni 10 Nukta 5 za Kimarekani Rais John Magufuli alipokutna na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,-Borge Brende  akiwa na  Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dr. Augustine Mahiga na wengine ni maafisa wa Serikali ya Norway. Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,-Borge Brende amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa nchi yake itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania hususani katika kuboresha huduma za kijamii na uwekezaji katika miradi mikubwa ya maendeleo. Brende ametoa dola za kimarekani milio...

CABALLERO JOINS CHELSEA FC TODAY

Picha
Trying to get a grasp of what has happened in football in last 24 hours? Check it out in our daily news summary.  TOP STORIE Official: Goalkeeper Willy Caballero today joins Chelsea Football Club  Caballero arrives having been out of contract at Manchester City. He will add strength to our goalkeeper resources following the departure of Asmir Begovic to Bournemouth.

CHILE OR GERMANY FINAL CONFEDERATION CUP

Picha
Chile or Germany: which team will Russia support? 1 hour ago / autty The FIFA Confederations Cup Russia 2017 has been extremely popular in the host country. Russian fans flocked to stadiums for the Tournament of Champions to cheer for the participating teams: the way the whole of the Saint Petersburg Stadium cheered for Cameroon during the group stage, for example, was unforgettable.  But who will Russians side with in today’s final: Chile or Germany? The world champions were stunned by the reception they received in Sochi to the point where the German Football Federation published a direct message to Russian fans from team captain Julian Draxler in Russian. The Chile team have also won favour with many Russian fans thanks to their colourful supporters, self-assured play and the heroics of Claudio Bravo in the penalty shootout against Portugal.