NORWAY YAIPATIA TANZANIA DOLA 1O.5 ZA KIMAREKANI
Norway yaipatia Tanzania Dola Milioni 10 Nukta 5 za Kimarekani
Bunge la Tanzania limesoma miswada mitatu inayohusu rasilimali za maliasili za nchi Sirro:
Ushirikiano wa dhati baina ya wananchi na dola unahitajika kukomesha mauaji Pwani.
Taifa Stars kumenyana na Afrika Kusini katika robo fainali ya COSAFA
Ujerumani na Chile zatinga fainali ya michuano ya kombe la mabara
Posted : July 02, 2017 (today) By Costamalimbwi
Norway yaipatia Tanzania Dola Milioni 10 Nukta 5 za Kimarekani
Rais John Magufuli alipokutna na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,-Borge Brende akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dr. Augustine Mahiga na wengine ni maafisa wa Serikali ya Norway.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,-Borge Brende amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa nchi yake itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania hususani katika kuboresha huduma za kijamii na uwekezaji katika miradi mikubwa ya maendeleo.
Brende ametoa dola za kimarekani milioni 10.5 kutekeleza awamu ya tano ya mpango wa kuboresha mamlaka ya mapato nchini -TRA unaotarajia kuanza Julai mosi mwaka huu. Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Norway hakusita kumpongeza Rais Magufili juhudi anazozifanya katika kupambana na rushwa, kukabiliana na matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusimamia vizuri uchumi na shughuli za maendeleo.
Maoni
Chapisha Maoni