Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

WANANCHI KENYA WAANZA KURUDI KAZINI

Picha
Hali ya kawaida imeanza kurejea katika miji mingi nchini Kenya baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa Ijumaa. Watu wanaonekana kupuuza wito kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa kususia kazi leo kuomboleza watu waliouawa katika makabiliano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wanapinga matokeo ya uchaguzi wa urais. Wiki iliyopita, biashara nyingi zilifungwa watu wakihofia kuzuka kwa fujo kutokana na uchaguzi uliofanyika Jumanne. Baadhi ya maeneo yakiwemo mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na maeneo ya magharibi mwa Kenya yakiwemo Kisumu, Homa Bay na Migori. Odinga awataka wafuasi wake kususia kazi Kenya Kofi Annan amtaka Odinga kutumia njia za kisheria Kenya Tofauti na hali ilivyokwa Ijumaa, biashara zimeanza kufunguliwa na magari ya uchukuzi wa abiria yameanza kufanya kazi katika barabara nyingi. Baadhi ya wakazi mtaani Kibera wameambia BBC kwamba wanahitaji kufanya kazi kujipatia chakula na mahitaji mengine ya kimsingi. Lakini wengine wameamua kutekeleza ushauri wa...